HOSPITALI ya Mkomaind imenunua mashine ya X-ray
16 March 2021, 4:08 AM
HOSPITALI ya Mkomaindo iliyopo halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara imenunua mashine tatu za kisasa ikiwemo mashine ya X-ray ambayo ni Digital X-ray Mashine ambapo mashine hizo tatu zina thamani ya sh.161 milioni lengo likiwa ni kuboresha upatikanaji wa huduma za afya hospitalini hapo. Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Masasi, Peter Majura aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Majura alieleza kuwa fedha za ununuzi wa mshine hizo zitatokana na fedha za mapato ya ndani ya hospitali hiyo baada ya hospitali hiyo kuingia mkopo na Bima ya Afya ( NHIF) kwa ajili ya ununuzi wa machine hizo matatu kwa dhamira ya uboreshaji wa huduma za afya ikiwemo huduma ya X-ray Alizitaja mashine hizo tatu zilizonunuliwa na hospitali hiyo kuwa ni mashine ya X-ray, mashine ya usingizi kwa ajili ya mgonjwa anapofanyiwa upasuaji na mshine ya kutakasa vifaa tiba mbalimbali vinavyotumiwa na madaktari wakati wa kutoa huduma za afya kwa wagonjwa. Majura alieleza kwamba kwa upande wa mashine ya X-ray iliyonunuliwa ina uwezo mkubwa wa kutoa huduma kwa wagonjwa wapatao 200 kwa siku ukilinganisha na uwezo wa mashine ya zamani iliyopo na kwamba kwa sasa mashine hizo zote mbili zitakuwa zikitumika kwa pamoja ili kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa huduma hiyo ambayo na kuongeza ufanisi wa huduma hizo za afya kwa wananchi. Hospitali ya Mkomaindo inaendelea kuboresha huduma zake zote za afya ili kila mwananchi ambaye anakwenda kupata huduma aweze kuhudumiwa ipasavyo