TAASISI ya (TaTeDo) kwa kushirikiana na Shirika la WWf watoa mafunzo wajasiliamali wadogo
4 March 2021, 4:12 AM
TAASISI ya kuendeleza Nishati Asili Tanzania (TaTeDo) kwa kushirikiana na Shirika la WWF wameanza kutoa mafunzo kwa wajasiliamali wadogo wanawake zaidi ya 20 kutoka katika vikundi 10 wilayani Masasi mkoani Mtwara ya kuwajengea uwezo wa umuhimu wa matumizi bora ya Nishati isiyo tokana na miti na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa Nishati ambazo zinachangia katika uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu ya Tanzania. Aidha,wajasiliamali hao wadogo pia wamefundishwa jinsi ya kutumia majiko sanifu na utengenezaji bidha mbalimbali za vyakula ikiwemo keki,skonzi na mikate kwa kutumia mkaa na kuni kwa kiasi kidogo mafunzo ambayo yatawasaidia kuweza kujiinua kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato. Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika wilayani Masasi mkoani hapa na kusimamiwa na Halmashauri mbili zilizopo wilayani Masasi, Halmashauri ya mji Masasi pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Masasi.