Micheweni FM
Micheweni FM
26 August 2025, 9:35 am

Huduma ya chanjo ni kipaombele kikuu cha serikali ambapo chanjo hizo ni salama na zimethibitishwa na shirika la afya duniani (WHO)pamoja na wizara ya afya kupitia wakala wa chakula, dawa na vifaa tiba ,hivyo hakuna sababu ya kuhofia kupata chanjo hizo
Na Mwiaba Kombo
Waandishi wa habari kisiwani Pemba wametakiwa kutumia taaluma yao ya habari katika kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa huduma ya chanjo.
Kauli hiyo imetolewa na meneja wa mpango wa chanjo wa taifa Zanzibar kutoka wizara ya afya Abdul-hamid Amir Saleh wakati alipokuwa akifunga mafunzo kwa waandishi wa habari kisiwani humo na kuwataka kuendelelea kushirikiana ili kuweza kuibua changamoto ambazo zipo katika jamii .
Kwa upande wake mratibu wa chanjo kisiwani Pemba Bakari Hamad Bakari amesema waandishi wana nafasi kubwa ya kuhakikisha kila muhusika anapata chanjo ambayo imekusudiwa kwake .
Aidha amewataka waandishi hao kutoa elimu kwa jamii ili kumaliza chanjo bila ya kukatisha njiani na kuacha dhana potofu ambazo zinatolewa na baadhi ya wajamii kususia huduma hiyo hasa kwa watoto .
Nae afisa chanjo kitengo shirikishi cha mama na mtoto Zanzibar Ruzuna Abdulrahim Mohd ameeleza kuwa chanjo hizi ni salama na kuwataka waandishi hao kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii juu ya masuala ya chanjo kila fursa inapopatikana.
Saut ya afisa chanjo kitengo shirikishi cha mama na mtoto Zanzibar Ruzuna Abdulrahim Mohd
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema elimu ambayo wameipata wataifanyia kazi kwa vitendo na kuhakikisha jamii inapata elimu kuhusu umuhimu wa chanjo
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika ukumbi wa Maktaba Chake Chake Pemba ambapo umewashirikisha waandishi mbali mbali wa vyombo vya habari kisiwani humo pamoja na watendaji wa wizara ya afya.