Loliondo FM
Loliondo FM
8 June 2025, 9:08 pm

Mifuko na chupa za plastiki ni uchafu ulio hatari zaidi kwa mazingira hasa zikitumika na kutupwa ovyo hususani kwa wilaya ya Ngorongoro inaweza kuleta madhara makubwa kwa mifugo na wanyama endapo wataila na kuimeza.
Na Zacharia James
Wananchi wilayani Ngorongoro wamehamasishwa kudhibiti matumizi ya bidhaa za plastiki ikiwemo mifuko na chupa ili kupunguza uhatari wake kwa mazingira na kuzuia vifo vya mifugo na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Mwl. Thomas Nadeade Juni 5, 2025 wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kiwilaya yaliyofanyika katika shule ya sekondari Loliondo yaliyoambatana na kilele cha kongamano la 6 la malihai likihusisha wanafunzi 100 kutoka shule mbalimbali wilayani hapa kutoka klabu za utunzaji wa mazingira kujadili,kutathmini na kuweka mikakati thabiti na shirikishi ya kukomesha matumizi ya bidhaa hizo sambamba na na ziara ya kitalii na mafunzo katika hifadhi ya taifa Serengeti kujifunza uhifadhi wa uoto,ikolojia ya viumbe na maliasili.
Mwl. Nade amewasihi wanafunzi kuwa kioo kwa jamii na mabalozi wazuri wa mazingira kwenye maeneo yao kwani wanauelewa wa kutosha juu ya mbinu za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira huku akiisihi jamii hasa ya kifugaji wilayani Ngorongoro kuepuka kununua na kutumia na kasha kutupa mifuko na chupa za plastiki kwani kama zilivyohatari kwa uhai wa mifundo ndivyo zilivyo na madhara kwa mazingira kwa kutorusu rutuba ,kutoruhu maji kupenya arthini na kutooza ,huku akilishukuru shirika la Frankfurt zoological society kwa kufadhili kongamano hili na kuendeleza juhudi za uhifadhi wa mazingira na maliasili nyingine kupitia miradi mbalimbali wanayoitekeleza katika eneo la ikologia ya Serengeti.
Kwa upande wake afisa maendeleo ya uhifadhi shirika la Frankfurt Zoological Society Nelson Ole Kuwai amesema shirika hili linashirikiana na shirika la hifadhi za taifa Tanzania yani TANAPA kuendeleza uhifadhi na sasa shirika linahudumu katika nchi 6 za kiafrika lengo kuu likiwa ni kupunguza uhasana na kuleta usawa baina ya wahifadhi wa wanyama na wananchi wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi kwa kuwawezesha katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujuzi,vifaa na mbinu za kujiinua na kujikwamua kiuchumi.
Mwalimu Rugano Adam Mwansansu mwenyekiti wa walimu walezi wa malihai klub kwa wilaya ya Ngorongoro ameitaka jamii kuungana na kushirikiana kwa pamoja ili kutunza mazingira kwa kupanda miti ,kutunza vyanzo vya maji,kutotupa taka hovyo na kupumguza matumizi ya vifaa na vyombo vya plastiki kama kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira mwaka huu inavyohimiza ,kwani vinamadhara makubwa kwa viumbe hai hususani wanyama pori na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inategemewa kwa uchumi wa wananchi wa wilaya hii ya Ngorongoro.
Naye mwnafunzi Debora Emmanuel Sesat kutoka Loliondo sekondari anaonyesha furaha yake kwa kulishukuru shirika hili kwa kufadhili kongamano hili na kugharamia safari ya kutalii katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.