Ileje FM

RC Songwe aridhishwa na ujenzi daraja la Msangano

September 18, 2025, 6:34 am

Mkuu wa mkoa wa Songwe Jabiri Omary Makame akikagua ujenzi wa daraja la Msangano.(Picha na Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde,Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omari Makame amepongeza maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Msangano Chindi, daraja kubwa linalojengwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 2.99.

Daraja hilo linajengwa katika Kata ya Msangano na litakuwa kiunganishi muhimu kati ya Halmashauri ya Momba, Mji wa Tunduma na Halmashauri ya Mbozi.

Pongezi hizo zilitolewa wakati Makame alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kujitambulisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba. Amesema maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ni ya kuridhisha na yanaendelea kwa kasi nzuri.

Mkuu wa Mkoa ameonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kuwataka TARURA kuhakikisha unakamilika ifikapo tarehe 25 Oktoba 2025, ili daraja liweze kuanza kutumika na kuondoa changamoto ambazo wananchi wamekuwa wakizipata hususan kipindi cha masika.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame
Ujenzi wa daraja la Msangano lililopo kijiji cha Chindi wilayani Momba.Picha na Denis Sinkonde