Ileje FM
Ileje FM
September 15, 2025, 9:37 am

Na Denis Sinkonde
Chama cha mapinduzi kata ya Mlale wilayani Ileje Mkoani Songwe kimezindua rasmi kampeni za kusaka kura za udiwani kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29 2025.
Uzinduzi wa kampenzi hizo umefanyika Septemba 14 mwaka huu katika Kijiji cha Iyuli katika kata hiyo huku wananchi wakitarajia kutatuliwa changamoto zinazowakabili ikiwepo maji.
Sauti za wananchi kata ya Mlale

Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Mlale kupitia chama hicho Yotham Ndile akinadi sera na ilani ya chama hicho amesema.
“Mimi sina fedha za kujengea miradi niwaahidi nitahakikisha nawaleta watalamu mkawaulize kwanini hamtatui changamoto zetu, kwani mimi mshenga mmenikuta niko vizuri,” amesema Ndile
sauti ya mgombea udiwani kata ya Mlale
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo mjumbe wa kamati ya siasa na mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake (UWT) Groly Mjema wilaya ya Ileje ameelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita.
sauti ya mwenyekiti UWT wilaya ya Ileje
Maeneo mengine ambayo chama hicho kimefanya uzinduzi kusaka kura kwa nafasi za udiwani ni Pamoja na kata ta Itale ambapo mgombea udiwani nafasi ya udiwani kata hiyo Fahari Mwampashi amenadi sera zake kwenye Kijiji cha Ishinga.