Ileje FM
Ileje FM
June 18, 2025, 3:03 pm

Mikakati hiyo ya serikali imetajwa kuwa itasaidia kukabiliana na wimbi la udumavu,utapiamlo na ukondefu hususani kwa watoto chini ya miaka 5
Na:Joel Kibona
Serikali itaendelea kuimarisha ustawi wa jamii kupitia utekelezaji wa agenda ya lishe bora kwa watoto, ili kukabiliana na changamoto za udumavu, utapiamlo na ukondefu.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwajenga watoto kuwa kizazi bora chenye afya njema na mchango chanya kwa taifa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi , Juni 17, 2025, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji yaliyofanyika katika kijiji cha Ilulu, kata ya Isongole, wilayani Ileje, ambapo aliwapongeza wazazi kwa kujitokeza kwa wingi kujifunza kuhusu lishe bora kwa watoto.
Amesema wazazi wanapaswa kutumia fursa hiyo kuhakikisha watoto wanapata lishe kamili kila siku.

Amewahimiza wazazi kushirikiana kwa pamoja na kuzingatia lishe bora kwa watoto wao, akisisitiza kuwa Wilaya ya Ileje imejaliwa ardhi yenye rutuba inayotoa mazao bora yenye virutubisho muhimu kwa ukuaji wa watoto.
Mgomi amewapongeza wanawake wa kijiji cha Ilulu kwa kujitoa siku ya lishe kuifanya siku ya lishe kuwa ya kipekee