Ileje FM
Ileje FM
June 11, 2025, 1:21 pm

Usimamizi wa fedha za mradi usipofuata taratibu baada ya mabazara ya madiwani kuvunjwa kutaibuka miradi mingi haitakamilika kwa wakati ukilinganisha na malengo ya serikali na kuibua hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.
Na:Denis Sinkonde
Ileje.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewataka wakuu wa idara na vitengo katika halmashauri za mkoa wa Songwe kusimamia na kufuata utaratibu wa kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hata baada ya mabaraza ya madiwani kuvunjwa.
Chongolo ametoa wito huo wakati wa kikao cha baraza la madiwani katila halmashauri ya Ileje lililofanyika kwa ajili ya kujadili hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).
Chongolo amewataka wataalamu wanaobakia kutekeleza majukumu ya kitaalamu kuvunjwa kwa mabaraza ya madiwani wasitumie kama mwanya wa kufanya mambo kiholela bali kuhakikisha fedha zinalindwa zaidi ambapo kila mkuu wa idara anatakiwa ajibadilishe kuwa diwani kulinda fedha za serikali na kuziba mianya ya ufujaji wa fedha hizo.
Sauti ya Daniel Chongolo mkuu wa mkoa wa Songwe
“Tuna vyombo vya usalama ambavyo vimechanganyikana na kuangalia matumizi ya fedha za serikali akiwepo Taasisi ya kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkuu wa wilaya ambaye ni mkuu wa shughuli za serikali pamoja Katibu Tawala amabye ni mjumbe wa baraza la madiwani na vikao vya wakuuwa idara wa halmashauri (CMT) anatikwa kuangazia macho yote kwenye vikao vya halmashauri kujuwa kila kitu kinaenda sawa,”amesema Chongolo.

Chongolo ameipongeza halmashauri ya Ileje kwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe