Ileje FM

RC Songwe awatahadharisha wazazi wanaowaozesha wanafunzi

May 9, 2024, 7:29 am

Katika habari ni mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kikota kata ya Ikinga hawapo pichani( Picha na Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde,Songwe

Katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, ametoa tahadhari kwa wazazi na walezi pamoja na wananchi kwa ujumla wilayani Ileje, mkoani humo wanaoendekeza vitendo vya kufungisha ndoa mabinti wenye umri mdogo, wakiwemo wanafunzi hali ambayo imekuwa chanzo cha mabinti wengi kukatisha masomo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Ikinga, wilayani humo katika moja ya mkutano wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amesema katika kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekithiri mkoani hapa.

Chongolo amesema  serikali haitawafumbia macho watu wote wanaondekeza vitendo hivyo “Tukikubaini ulishiriki kula ule wali pale kwenye ile shughuli na wewe umeshiriki yule mtoto kuharibiwa, kwa hiyo tutasomba wote.

Serikali inatoa fedha kuboresha miundombinu ya shule ili watoto wasome lakini wanaharibiwa ndoto na wazazi na walezi kwa kuwaozesha wote tutawakamata pamoja na watakaohudhuria harusi tutakamata wote,” amesema Chongolo.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo