Triple A FM
Triple A FM
16 July 2025, 12:13 pm

Tumeshapata viti karibia 300 ambavyo vitakuja kuwekwa kwenye majukwaa haya…..uwanja huu utakuwa wa tofauti sana….malengo yetu ni hata mechi za Afcon zije kufanya mazoezi ya AFCON
Joel Headman
Uchumi wa mji wa Babati umepanda kwa kasi hadi kuzidi malengo yaliyowekwa na Halmashauri hiyo iliyopo mkoani Manyara.
Akizungumza katika mahojiano maalum ya na kwa ana na redio Triple A yaliyofanyika mjini Babati mkuu wa wilaya hiyo bi.Emmanuela Kaganda ameutaja mchezo wa mpira wa miguu kuwa miongoni mwa nyenzo zilizotumika kupaisha uchumi wao
Katika mazungumzo yake amesema kuwa uwepo wa Timu ya Fountain Gate wilayani hapo umesaidia pakubwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na wilaya kwa ujumla.
Ameeleza kuwa kutokana na timu hiyo ya ligi kuu kuponea chupuchupu kushuka daraja wameamua kuwekeza nguvu kubwa Zaidi kuhakikisha inakua kwenye nafasi nzuri msimu ujao ikiwa ni pamoja na kufunga viti vya kukalia katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa ambao umekuwa ukitumiwa na Fountain Gate kama uwanja wao wa nyumbabni.