Radio Fadhila

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Masasi wamepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2021/2022

3 Machi 2021, 11:44 mu

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara wamepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 yenye Makadirio ya Mapato na Matumizi yenye thamani ya Sh.bilioni 19,651,959, 451.00 Bajeti hiyo wamepitisha jana ,Machi 2/2021 katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha Mpango huo wa bajeti kikoa hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Akisoma Bajeti hiyo mbele ya Madiwani hao Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Abdillah Mfinaga amesema kuwa katika Bajeti hiyo kati ya fedha hizo ruzuku ya mishahara ni Sh.bilioni, 13, 604, 188, 500.00 Amesema kuwa ruzuku ya matumizi mengineyo Sh.bilioni 2,522, 289,201.00. Ruzuku ya miradi ya maendeleo ni Sh.3, 525, 481, 750.00 fedha zinazotokana na Mapato ya ndani ni Sh.1, 575,805,500.00 fedha za Mapato ya nje ni Sh.1, 949,676,250.00 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Gimbana Ntavyo ameahidi kuendelea kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani kwa ufanisi uliobora bora. Ambapo amewataka wadau mbalimbali kutoa ushirikiano wa karibu na Halmashauri hiyo ili kufanikisha kuijenga Masasi.

chanzo -Hamisi Abdelehemani Nasiri