Radio Fadhila

WATUMISHI wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, wametakiwa kutumia utaalamu wao ili kuisaidia Halmashauri hiyo

17 Disemba 2020, 11:19 mu

WATUMISHI wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, wametakiwa kutumia utaalamu wao ili kuisaidia Halmashauri hiyo kuweza kupiga hatua ya kimaendeleo, ikiwemo kubuni vyanzo vipya vya mapato Aidha, watumishi hao wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wajikite zaidi katika kuisukuma Halmashauri kwa kushirikiana bega kwa bega na madiwani katika kuwahudumia wananchi kwa kutatua kero zao Wito huo umetolewa leo wilayani Masasi na Madiwani wa Halmashauri hiyo katika kikao cha kuapishwa rasmi kilichofanyika katika kijiji cha Mbuyuni ziliziko ofisi za Halmashauri hiyo.Madiwani hao waliyataja maeneo ambayo ni kipaumbele wanayokwenda kuyatekeleza ni elimu, maji, afya, uchumi na kilimo ambapo maeneo hayo bado kumekuwa na changamoto nyingi zinazoikwamisha Halmashauri kushindwa kupiga hatua ya kimaendeleo. Pia Madiwani wa Halmashauri hiyo leo wamemchagua rasmi mwenyekiti mpya wa Halmashauri hiyo pamoja na makamu mwenyekiti , ambapo nafasi ya mwenyekiti amechaguliwa diwani wa kata ya Mpeta, Ibrahimu Chiputula na makamu mwenyekiti amechaguliwa diwani wa kata ya Msikisi, Anthony Chihako.-

chanzo-Hamisi Abdelehemani Nasiri