Micheweni FM
Micheweni FM
5 September 2025, 11:09 am

Wananchi kisiwani Pemba wamesema hawajawahi kushuhudia maendeleo makubwa kama yale yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Na Mwiaba Kombo
Wakizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar waliotembelea miradi mbalimbali kisiwani humo, wananchi hao wamesema utekelezaji wa miradi hiyo ni kielelezo cha utekelezaji mzuri wa ahadi za serikali.
Khatib Mjanawe Arafa, mkazi wa kijiji cha Maziwang’ombe, amesema wananchi wa kijiji hicho wanajivunia hatua za maendeleo zilizofikiwa na wameahidi kumpa kura nyingi Dkt. Mwinyi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Naye Alawia Hamadi Ali, pia kutoka kijiji hicho, amesema wananchi walikuwa na hamu kubwa ya kuona maendeleo, na kwamba ujio wa Dkt. Mwinyi umewezesha miradi mingi muhimu kutekelezwa katika kijiji chao.
Wananchi hao wamesema wako tayari kumuona Dkt. Mwinyi akiendelea kuiongoza Zanzibar kwa miaka mingi zaidi, wakisisitiza kuwa ndiye chaguo sahihi kwao.