TRA Pemba yawatembelea wafanyabiashara yasikiliza changamoto zao
18 December 2024, 6:24 pm
meneja mamalaka ya mapato TRA mkoa wa kikodi pemba Arif Said akizungumza na mfanya biashara katika maeneo ya duka kiswani pemba ikiwa ni ziara maalum ya kuwatembelea na kusikiliza changamaoto zinazowakabili ikiwa ni ziara maalumu ya kuwatambelea wafanya biashara kwa lengo la kujua changamoto zinazo wakabili. Picha na Essau Kalukubila.
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili katika maswala mbali mbali ya ulipaji kodi ndani ya biashara zao
Na Essau Kalukubila.
Wafanya biashara kisiwani pemba wametakiwa kuendeleza mashirikianio na mamlaka ya mapato Tanzania TRA ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili katika maswala mbali mbali ya ulipaji kodi ndani ya biashara zao .
Akizungumza na wafanya biashara katika maeneo mbali mbali ya maduka kiswani pemba ikiwa ni ziara maalum ya kuwatembelea na kusikiliza changamaoto zinazowakabili ikiwa ni ziara maalumu ya kuwatambelea wafanya biashara kwa lengo la kujua changamoto zinazo wakabili meneja mamalaka ya mapato TRA mkoa wa kikodi pemba Arif Said amewataka kwendelea kulipa kodi kwa wakati ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.
Nao wafanya biashara hao akiwemo Ahmed Said pamoja na juma shabani maalim pamoja na kuishukuru mamalaka hiyo kwa kuwatembelea wameispongeza serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanya biashara ikiwemo kuimarisha bandari bandari ya mkoani na kuweza kushusha makontena moja kwamoja hali ambayo imeondoa usumbufu ulio kuwepo awali ikiwemo kukosa tenda za kuagiza bidhaa .