Wanawake watakiwa kuzigeuza changamoto kuwa fursa michezoni
25 November 2024, 10:57 am
Changamoto ni mazingira kinzani ya upinzani kwenye kila nyanja yanayokuja katika maisha yako ambapo kwa jina jengine tunaiita matatizo ambalo neno hili ni baya kwa watu wengi katika jamii neno hili linajumuisha matatizo ya kiuchumi ,kijamii na kisiasa ,lakini leo tutazungumza Zaidi changamoto kwenye jamii katika suala zima la michezo .
Na Mwiaba Kombo.
Makala maalum ambapo kwa siku ya leo tutazungumzia changamoto ambazo wanakumbana nazo wanawake katika suala la michezo Mkoa wa kaskazini Pemba ambapo Makala hii inaletwa kwako na Mwiaba Kombo Hamad, kwa ushirikiano wa Chama Cha Waandishi Wa Habari Wanawake, Tanzania, Zanzibar (TAMWA Zanzibar), kupitia mradi wa Michezo kwa Maendeleo unaotekelezwa chini ya ufadhili shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ) nikusihi tuwe pamoja mwanzo hadi mwisho wa Makala hii