Madiwani halmashauri ya wilaya ya Micheweni watakiwa kufuatilia miradi katika wadi zao
20 November 2024, 1:15 pm
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Micheweni wamefanya kikao cha mwanzo wa mwaka 2024-2024 ili kujadili ripoti ya kamati mbali mbali ambazo zimefanya ziara kwa lengo la kuangalia ni kwa namna gani halmashauri inaweza kuboresha mapato yake kupitia vyanzo vyake vya mapato
Na Mwiaba Kombo
MADIWANI katika halmashauri ya wilaya ya Micheweni wametakiwa kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo katika wadi zao.
Akizungumza baada ya kumaliza kikao cha ripoti ya mapato na matumizi cha kwa kipindi cha mwezi Julai –September 2024 makamu mwenyekiti wa kamati ya baraza la madiwa ambae pia ni diwani wa wadi ya Micheweni Bakari Mjaka Faki amesema lengo la kikao hicho ni kuona ni kwa kiasi gani mapato na matumizi katika halmashauri hiyo yanatumika.
Amesema ni jukumu la kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha aasimamia vyema majukumu yake ile lengo la serikali katika suala la maendeleo liweze kufikiwa
Kwa upande wake katibu wa baraza hilo ambae pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Micheweni Hamad Mbwana Shehe amewataka wananchi kuendelea kuwa na Imani nao na kuendelea kulipa ada na tozo ambazo zinastahiki ili waweze kuletwa maendeleo kupitia halmashauri hiyo.
Amesema endapo wananchi watachangia mapato katika halmashauri hiyo ni Dhahiri maendeleo yataeza kufikiwa haraka katika maeneo yao
Nao diwani wa viti maalum kupita jimbo la Wingwi Saumu Mohd Said pamoja na diwani wa wadi ya Tumbe Ali Juma Shaibu wamesema ni jukumu la madiwani pamoja na mafisa wengine wa halmashauri kushirikiana kwa pamoja ili malengo yaweze kufikiwa.