THRDC watoa msaada wa magodoro gereza la Loliondo
5 November 2024, 11:29 am
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania ni miongoni mwa wadau muhimu wa kutetea haki za binadamu hapa nchini sambamba na hilo wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli zingine za kijamii ikiwepo kutoa misaada mbalimbali ya huduma muhimu za kijamii katika makundi maalum mfano magereza.
Na Edward Shao
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na kituo cha msaada wa kisheria Ngorongoro (NGOLAC) watoa msaada wa magodoro gereza la Loliondo wilaya ya Ngorongoro.
Akizungumza katika gereza la Loliondo mratibu wa THRDC bw Onesmo Ole Ngurumwa Novemba 04, 2024 amesema wametoa msaada wa magodoro hayo kwa lengo la kuboresha malazi ya watuhumiwa pamoja na wafungwa pale wanapoona kuna changamoto na siyo Tanzania bara pekee hata Zanzibar licha ya kukosoa baadhi ya mienendo Ila bado wamekuwa sehemu ya kusaidia jamii.
Amesema wao kama THRDC na NGOLAC wataendelea kujenga mahusiano mazuri na taasisi kama magereza kwani serikali hawawezi kukamilisha mahitaji yote kwa wakati mmoja huku akitoa pongezi kwa gereza la Loliondo kwa kulikuta likiwa katika ubora unaotakiwa ikiwepo usafi,kutokuwa na msongamano wa wafungwa na hata wanakolala huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia mahitaji mengine kama vile chakula,malazi na huduma nyingine.
Bw Onesmo pia amesisitiza uongozi wa gereza hilo kuendelea kuwasimamia wafungwa katika misingi ya haki za bidadamu na kuwepo wa kitengo cha msaada wa kisheria gerezani kwa wafungwa watakaohitaji msaada wa kisheria.
kwa upande wake mrakibu wa magereza George Osindi mkuu wa gereza Loliondo wilaya ya Ngorongoro ameshukuru THRDC na NGOLAC kwa msaada wa magodoro 10 kama kianzio huku akiomba wadau wengine wa maendeleo ndani au njee wa wilaya ya Ngorongoro kuwafikia na kutoa misaada kama hiyo.
Gereza la Loliondo linatajwa kuwa gereza la tatu kwa ukongwe hapa nchini lenye historia kubwa baada ya megereza yaliyopo Biharamulo na Tanga likijengwa na kuanzishwa mwaka 1922.