Makonda na ziara ya kwanza Ngorongoro
2 July 2024, 2:03 am
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Makonda amefika walayani Ngorongoro kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Zacharia James.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Makonda amesema zaidi ya wananchi milioni moja ndani ya mkoa wa Arusha watanufaika na miradi ya maji katika maeneo yao vikikamilika visima 37 wilayani Ngorongoro kati ya vingi mkoani hapa.
Ameyasema hayo leo Julai Mosi 2024 akiwa wilayani Ngorongoro katika ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na wakala wa maji mijini na vijijini ruwasa kwa ufadhili wa umoja wa falme za kiarabu (UAE) ambapo mbali na kuwashukuru wafadhili hao amempongeza rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.samia suluhu Hassan kwa kufanikisha mahusiano mazuri na mataifa mengine mahusiano yanayopelekea wahisani hawa kusaidia wananchi kupata huduma hii muhimu ya maji katika maeneo yao.
Mhe. Makonda amewasihi viongozi ngazi za jamii na wananchi kwa ujumla kuwa walinzi madhubuti na kuitunza miradi hio ya maji ili ikafikie malengo yaliokusudiwa wa kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata mbali huduma ya maji pia amewatowa hofu wafugaji kwamba miradi hio mbali na kurahisisha upatikanaji wa maji kwa binadamu pia miradi hii itatoa nafasi kwa mifugo kunywa maji katika maeneo yaliyotengwa jirani na miradi hio huku akiagiza maji yafike katika maeneo yote yenye makazi ya watu hasa wanaoishi maeneo ya vijiji vilivyo katika maeneo magumu kufikika hasa Oloboo huku akiomba wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wakati wa utekelezwaji wa miradi hiyo ya maji.
Miradi hii inatekelezwa kwa ufadhili wa utawala wa falme za kiarabu ambapo wilayani hapa vimechimbwa visima 18 kati ya hivyo 12 vinatoa maji huku katika ziara hio mkuu wa mkoa amekagua visima vilivyopo Oloboo,shule ya msingi Wasso,Maaloni na uchimbaji wa kisima Sale mbali na ukaguzi huo wa visima vya maji mkuu wa mkoa Makonda amewaahidi wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kua atakua na ziara rasmi ya kuskiliza kero za wanachi maarufu kama ziara ya kupiga spana wilayani hapa katika kipindi kifupi kijacho.