Loliondo FM

Ole Shangai ashukuru kwa miaka minne ya heshima Ngorongoro

29 July 2025, 7:27 pm

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai picha na mpiga picha.

Chama cha mapinduzi (CCM) kinaendelea na mchakato was kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu utakofanyika oktoba mwaka huu 2025 ambapo kwasasa chama hicho kipo katika mchakato wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge.

Na Edward Shao

Leo, tarehe 28 Julai 2025, mbunge wa Jimbo la Ngorongoro anayemaliza muda wake Mhe Emmanuel Ole Shangai kupitia ofisi ya mbunge ametangaza kupokea maamuzi ya chama kuhusu wagombea wa uchaguzi wa ubunge baada ya jina lake kuondolewa kwenye orodha majina ya kura za maoni wa chama cha mapinduzi CCM Jimbo la Ngorongoro.

Mhe. Emmanuel Ole Shangai amewashukuru wananchi wa kata ya Endulen na jimbo zima la Ngorongoro kwa kumpa ridhaa ya kumteua kuwa diwani kwa miaka 10 na mbunge kwa kipindi cha miaka minne akihitaja kuwa ni heshima kubwa kwake na kwa wananchi kwa ujumla.

Mbunge huyo amesema amejitahidi kuwawakilisha wananchi vyema na kuleta miradi ya maendeleo inayogusa maisha yao kwa njia nzuri na ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi katika harakati za maendeleo pamoja na kuimarisha chama chake.

Katika hatua nyingine, chama cha mapinduzi (CCM) kupitia kwa katibu wa NEC, Itikafi, uenezi na mafunzo, CPA Amos Makalla jijini Dodoma, leo Julai 28 2025 kimetaja majina sita ya wagombea wanaoomba ridhaa ya ubunge katika jimbo la Ngorongoro, ikiwa ni pamoja na wanawake wawili.

Majina 10 ya wagombea yalielekezwa kamati kuu ya CCM kwa ajili ya uchaguzi wa jimbo la Ngorongoro na baada ya uchambuzi na mchujo wa chama, majina sita kati yao yamepita kusubiri kura za maoni kuwania kiti cha ubunge jimbo la Ngorongoro majina hayo ni Ndg Yannick Ikayo Ndoinyo, Ndg Rose Ormorijoy Njilo, Ndg Prof. Kokel Letia Melubo, Ndg Sylvanus Mizengo Ole Pinda, Ndg Marx Simon Kakaoni na Ndg Elizabeth Sinodya Gibaseya.