Loliondo FM

Viongozi serikali za mitaa wapewa mafunzo ya sheria na utawala bora Ngorongoro

18 March 2025, 9:38 pm

Mtaalamu kutoka wizara ya katiba na sheria akitoa mafunzo Kwa viongozi wa serikali za mitaa.

Katika kuhakikisha utendaji kazi Kwa viongozi wa serikali za mitaa wilayani Ngorongoro unakuwa na tija kwa wananchi, wizara ya katiba na sheria imewapatia viongozi hao mafunzo Kwa lengo la kuongeza ufanisi katika majukumu yao.

Na Saitoti Saringe

Wizara ya katiba na Sheria ikiongozwa na Wakili Joyce march 18, 2025 wametoa mafunzo ya sheria na utawala Bora kwa viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Wakuu wa Divisheni, Watendaji wa Kata pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ngorongoro.

Bw. Yohana Mcharo amewataka Watumishi wa Umma kila mmoja kutimiza wajibu wao, huku akiwahasa kuitambua kila mmoja anatekeleza majukumu yake kwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo wanatakiwa kuzingatia Sheria na utaratibu ili kuwatumikia Wananchi vyema bila kuwanyanyasa.

Mafunzo hayo yameangazia katika nyanja mbalimbali kama vile umuhimu wa Demokrasia, kuheshimu katiba, Sheria na haki za binadamu pamoja na umuhimu wa kufuata kanuni za utawala bora ili kuwafanya Wananchi kupata haki zao za kisheria pamoja na kupata maendeleo ikiwa na kutoa taarifa zote muhimu kwa wananchi ili kujenga na kuimarisha uhusiano kati ya Wananchi na Serikali.