Loliondo FM

Mimutie yaibua mapya kesi ya ulawiti mbele ya Makonda Ngorongoro

9 July 2024, 8:46 am

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh Paul Makonda picha na mpiga picha wetu.

Matukio ya ukatili kwa mkoa wa Arusha yameendelea kushika kasi huku wadau wa kupambana na maswala hayo ya ukatili wakijitolea kutafuta haki kwa wahanga lakini imeonekana kukosa ushirikiano baina yao pamoja na vyombo mbalimbali vya kutoa msaada wa kisheria hali inayoonekana ni kikwazo kikubwa katika kutafuta haki.

Na Edward Shao.

Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe Paul Makonda ameshangaa kwanini kesi ya mtoto aliye lawitiwa iliyoibuliwa katika kliniki yake yakusikiliza kero za wananchi mkoani hapa kwanini haijafika mahakamani huku akiitisha kikao cha dharura Julai 9,2024.

Amesema hayo Julai 8,2024 wakati alipokutana na wadau mbalimbali katika kikao cha mrejesho na tathimini namna serikali inavyowahudumia wananchi mkoani Arusha.

Akihibua kesi hiyo ya ulawiti mkurugenzi mtendaji wa shirika la Memutie bi Rose Njilo ametoa lawama zake mbele ya mkuu wa mkoa, kwanini maagizo aliyoyatoa kuhusu kesi hiyo ya ulawiti hadi sasa haijafanyiwa kazi huku akisema kuna baadhi ya viongozi waliopewa maagizo hayo wamekuwa wakizungumza uongo kuhusu mwenendo wa kesi hiyo akimtaja mkuu wa wilaya ya Arusha mjini.

Ameongeza kuwa Memutie kwa kushirikiana na wadau wengine wa kupinga ukatili wamekuwa wakiangaika katika ofisi mbalimbali mkoani Arusha kutafuta haki ya mtoto huyo aliyelawitiwa lakini awajapata msaada hali inayopelekea mama mtoto kutaka kujiua.

Bi Rose Njilo ameongeza kuwa swala la ukatili kwa mkoa wa Arusha liko juu na wao kama wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wanashindwa kufanya kazi kutokana na kukosa ushirikiano kutoka jeshi la polisi.

Sauti ya Rose Njilo na Mkuu wa mkoa wa Arusha.