RAS Arusha aahidi kumleta Makonda Ngorongoro
22 June 2024, 5:58 pm
Kwa mujibu wa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha lengo la mkoa ni kufikia (single digit) yaani chini ya hoja kumi ambazo zimefikia lengo ni halmashauri 5 pekee.
Na Zacharia James.
Katibu tawala wa mkoa wa Arusha mhe. Massaile Albano Musa amezitaka halmashauri za mkoa wa Arusha kulipa madeni hasa makubwa zinazodaiwa na watumishi,watoa huduma ama wazabuni ili kusaidia wasifilisike ama kupunguza ari na mwamko wa kufanyakazi za kuletea halmashauri maendeleo.
Ametoa kauli hio leo june 22 2024 katika kikao cha kuskiliza hoja za mthibiti na mkaguzi mkuu wa serikali yan CAG kwa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro huku akiiagiza halmashauri ya Ngorongoro kuhakikisha inazishughulikia hoja hizo kwa kuzingatia ushauri uliotolewa na kamati ya fedha na ofisi ya mdhibiti na mkauzi mkuu wa hesabu za serikali katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Halikadhalika mhe.Musa ameitaka halmashauri kujipanga kikamilifu katika ukusanyaji wa mapato kwa kupanua wigo wa makusanyo na kubuni vyanzo vipya vya mapato akivitaja kama ndio silaha pekee kwa halmashauri kulipa madeni, kutekeleza miradi na mambo mengine ya maendeleo,huku akikiri kuifahamu changamoto inayoikabili halmashauri ya kutopokea mapato kutoka katika taasisi kama vile mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na OBC na kuwataka kuliwasilisha katika ngazi za juu ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo na kuipongeza halmashauri ya wilaya ya ngorongoro kwa kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala kwa ufanisi huku akisisitiza mshikamano kuelekea uchaguzi ujao na akiahidi kumleta mkuu wa koa wa Arusha mhe Paul makonda kwa ziara wilayani hapa.
Naye mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Murtallah Sadiki ameahidi kua hadi kufikia September mwaka huu hoja hizo zitakua zimemalizika kwakua hoja nyingi ziko katika utekelezaji pia ameelezea kua halmashauri kupitia wataalam wa vitengo na idara mbalimbali wamejipanga kuhakikisha mwaka ujao hoja hizo hazitajirudia na hakutokua na hoja kabisa kwa zile zilizo ndani ya uwezo wa halmashauri,huku akiainisha mikakati kadhaa ya vyanzo vya mapato kama kuboresha mazingiza ya utalii mlima Oldonyo lengai,kukusanya katika machimbo ya madini iliyopo talafa ya Sale na kuzungumza na kupata mapato kutoka makampuni kupitia ushuru wa huduma yani service levy na ameainisha mikakati ya kulipa madeni yote na kuomba ushirikiano wa wananchi kwani milango yake ipo wazi mda wote.
Naye ndg Valence Rutakyamirwa mkaguzi mkuu wa nje mkoa wa Arusha ameshauri halmashauri katika kutekeleza hoja zilizopo wanatakiwa kuwasilisha nyaraka na taarifa zinazotakiwa,kukamilisha majengo na kuuliza na kuomba ufafanuzi juu ya hoja ambazo hawaelewi msingi wake kwani hoja sio mtihani akisisitiza nia ni kuweka ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za umma huku akiainisha malengo ya mkoa ni kua na singo digit yani chini ya hoja kumi na halmashari tano tu ndizo zimefikia lengo ambazo ni Longido,Arusha dc, Meru na Karatu huku Ngorongoro ikiwa na zaidi kidogo kwani imebakiwa na hoja 11 mpya.
Baadhi ya hoja hizo ni pamoja na halmashauri kushindwa kukusanya mapato na kufikia lengo la makusanyo,kutokukusanya mapato ya viwanja sh mill 19.3 eneo la uwanja wa ndege,mapungufu ya utekelezaji wa miradi ya hifadhi ya ngorongoro hasa mkataba wa ufadhili wa maendeleo ya jamii kupitia baraza la wafugaji ,mkopo ambao haukurejeshwa akaunti ya amana,mapungufu yaliyoonekana katika udhibiti wa ndani,mapungufu ya uthibiti mifumo ya tehama,kutotumika kwa fedha kwaajili ya ukamilishaji wa miradi milioni 800.16 hasa ukamilishaji wa sekondari za Sale na hoja nyinginezo.