Mashindano ya UMISETA yashika kasi Ngorongoro
31 May 2024, 9:46 pm
Mashindano ya Umiseta imeendelea kuvutia wapenzi wengi wa soka wilayani Ngorongoro baada ya kukutanisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali na wadau wa soka wilayani hapo.
Na Saitoti Saringe
Mashindano ya Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISETA) leo tarehe 31 Mei, 2024, yameendelea kushika kasi katika Viwanja vya michezo vya Shule ya Sekondari Loliondo ambapo kwa Wilaya nzima ya Ngorongoro mashindano yanafanyika katika viwanja hivyo jumla ya kanda nne zimeshiriki kikamilifu ikiwemo Kanda ya Digodigo, Lake Natron, Serengeti na Ngorongoro ili kupata timu itayoiwakilisha Wilaya kimkoa.
Afisa Michezo Wilaya Bw. Ngoka amesema kuwa, lengo la kuwepo kwa mashindano haya kila mwaka ni kuendelea kuibua vipaji vya Wanafunzi kwa manufaa yao na Taifa. Jumla ya michezo iliyoendelea hii leo ni pamoja na mchezo wa mpira wa miguu kwa Wanaume, mpira wa pete (Netiboli) kwa Wanawake na mchezo kuruka vihunzi kwa Wanaume.
Ikumbukwe kwa Miaka mingi Serikali imeendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Michezo kwani ni miongoni mwa Sekta zinazotoa ajira kwa Vijana wengi wa kitanzania.