Loliondo FM

DED Ngorongoro awataka watumishi kushirikiana

30 May 2024, 12:47 pm

Bw. Murtallah Sadiki (DED Ngorongoro)

Ilikufanikisha maendeleo ya wananchi kwa weledi watumishi wa Halmshauri wametakiwa kuwa na umoja na ushirikiano katika kutimiza majukumu yao.

Na Saitoti Saringe

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Murtallah Sadiki Mbillu amezungumza na Watumishi wa Wilaya ya Ngorongoro katika Ukumbi wa Halmashauri tarehe 27 Mei, 2024.

Akizungumza na Watumishi hao Bw. Murtallah amesema atafanya ziara ya kuwatembelea katika Vituo vyao vya kazi ili kujua, kuona na kutatua changamoto zinazowakabili, kupata muda mzuri wa kushauriana kwa maslahi mapana ya Wilaya ya Ngorongoro.

“Niwaombe mpendane, mshirikiane ukimuona mwenzako mwenendo wake sio mshauri, pia zingatieni maadili ya utumishi wa Umma, zingatieni aina ya mavazi yananayotakiwa kuvaliwa na Mtumishi” amsema Bw. Murtallah

Aidha, Mkurugenzi amewaasa Watumishi kuwa na ushirikiano, upendo na umoja katika kutekeleza majukumu yao ya kiutumishi, pia ametoa mawasiliano yake ya moja kwa moja kwa Mtumishi yoyote atakayepatwa na changamoto, au jambo lolote la maendeleo aweze kumshirikisha na kumfikia kwa urahisi.

Ikumbukwe kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Paul Makonda katika kikao chake na watumishi wote wa uma wa mkoa huo aliwataka watumishi wote kuwa karibu na wananchi ili kutatua kero zao kwa ukaribu zaidi.