ALAT yaipongeza Ngorongoro
25 May 2024, 11:26 pm
Mbali na fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Ngorongoro kutoa serikalini pia kumekuwa na wadau wanaotoa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na halmashauri, wadau hao nikama vile KWF,TANAPA na wengineo.
Na Zacharia James
Jumuia ya tawala za mikoa na serikali za mitaa (ALAT) mkoa wa Arusha imekagua na kupongeza halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kwa kazi nzuri ya kutekeleza miradi ya maendeleo kikamilifu na kwa ubora mbali na kubaini kasoro na mapungufu kadhaa.
Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Arusha Dr Ujungu Salekwa amebainisha hayo leo Mei 25, 2024 wakati akizungumza na Loliondo Fm kuhusiana na dhumuni la ziara hio amesema ni kukagua na kupitia miradi mitatu ambayo ni shule ya sekondari Masusu inayojengwa kwa sh, milioni 584.2, zahanati ya Mdito inayojengwa na wahisani TANAPA na shirika la kijerumani kupitia KFW kwa gharama ya Tsh. Milioni 280 na jengo la utawala (la Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ) ambalo limekamilika kwa asilimia 96 likitumia zaidi ya bilioni 2.7.
Dr Ujungu ameshauri halmashauri kuwa zahanati ya Mdito kwa kushirikiana na wahisani wakamilishe ujenzi wa nyumba za watumishi(madaktari)akisisitiza ugonjwa unaweza mkuta mtu mda wowote hata usiku hasa kwa wajawazito na watoto, kwenye ujenzi ameshauri kuwekwe mifumo ya kuvuna maji,mifumo ya umeme,mifumo ya udhibiti moto,marekebisho ya milango,madirisha na uwekaji bora wa vigae.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambae pia ni mjumbe wa kamati hio Mhe.Marekani Bayo ameishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuwapatia fedha nyingi za kuboresha miundombinu na kuwapongeza wadau wa maendeleo kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo huku akieleza kua atashirikiana na mkurugenzi wa halmashauri ya Ngorongoro Ndugu Murtallah Sadiki pamoja na wataalamu kurekebisha kasoro na mapungufu yaliyopo katika miradi hio ili ikamilike kwa ufanisi na tija kwa wananchi wa wilaya hapa.
ALAT inaundwa na wenyeviti wa halmashauri ,wastahiki meya,wakurugenzi na madiwani kutoka halmashauri mbalimbali ambapo walioshiriki ni kutoka jiji la Arusha ,Arusha DC,Arumeru,Karatu,Longido,Monduli na Ngorongoro