Nape Nnauye awataka wananchi Ngorongoro kusimama na Samia
16 April 2024, 7:13 am
Baadhi ya wananchi wachache katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakiitumia mitandao yao vibaya ikiwemo kuwatukana na kuwachafua viongozi wa nchi kwenye mitandao hiyo kinyume na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,hivyo viongozi wa serikali wamekuwa wakiwasisitiza kuacha kufanya hivyo kwani ni kosa la kisheria na watachukiliwa hatua pale watakapobainika.
Na Edward Shao.
Waziri wa habari,mawasiliano na tekinolojia ya habari mh Nape Nnauye awataka wananchi Ngorongoro na nchini kwa ujumla kusimama na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Dr Samia Suluhu Hassan kwa kusema yale yote mema na kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Ameyasema hayo April 15,2024 wilayani Ngorongoro kwenye viwanja vya waziri mkuu mji wa Wasso katika afla ya uzinduzi wa vituo vya kurushia matangazo Tbc taifa na Bongo fm .
Mh Nape amesema baada ya kazi nzuri inayofanywa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia anawaomba watanzania wote waamue kwa pamoja kusimama na rais hususani kwa wale walioko kwenye mitandao ya kijamii kuanzia sasa waiambie dunia wanasimama na rais kwa mema aliyowafanyia.
Ametaja sababu ya kwanini watanzania kusimama na Samia kuwa ni pamoja na wafanyibiashara kufanya biashara bila usumbufu,uhuru wa vyombo vya habari,ujenzi wa miundombinu ya madarasa,elimu bure hadi kidato cha sita bila kusahau kupata mikopo kwa wanafunzi wa chuo kikuu, ujenzi wa miundombinu ya afya na uwepo wa vifaa vya matibabu na mengine mengi yaliyofanywa na rais Samia.