DC Ngorongoro na ziara ya kwanza
25 February 2024, 8:46 am
Miradi mingi ya maendeleo wilayani Ngorongoro inayotekelezwa kupitia ufadhili wa benki ya maendeleo ya Ujerumani (KFW) imegusa karibu kila sekta muhimu ikiwepo Afya,barabara pamoja na sekta ya elimu.
Na mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanal. Wilson Sakulo leo tarehe 24 Februari, 2024 ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia ufadhili wa benki ya maendeleo ya Ujerumani KFW kujionea na kukagua uimara hiyo inayoendelea kutelekelezwa.
Pia ameutembelea miradi barabara ya Mairowa-Njoroi yenye urefu wa km11.1 ambayo iko katika hatua ya umaliziaji barabara hiyo imetengewa bajeti ya shilingi bilion 1.987, kisha kukagua barabara ya Kirtalo yenye urefu wa km 12.5 inayotarajia kukamilika tarehe 6 April, 2024.
Mradi mwingne ni mradi wa Shule za Sukenya iliyopo kata ya Oloipiri yenye madarasa matatu yenye thamani ya shilingi 211,905,100.70 ambayo iko katika hatua ya umaliziaji.
Kanali Sakulo pia amekagua zahanati ya Njoroi yenye thamani ya shilingi 358, 803, 250.48, Shule ya msingi Soitsambu yenye vyumba vitatu vya madarasa kisha kumalizia ziara kwa kukagua zahanati ya Kirtalo yenye thamani ya shilingi
milion 358, 803, 250.48.
Sambamba na hayo Kanali Wilson Sakulo amewahimiza wahisani wa KFW kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kutoa shukrani kwa Mhe. rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mahusiano mazuri na mataifa mengine na kuruhusu wahisani kuja nchini na kufanya miradi ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania.
Sakulo atakuwa na ziara maalum ya siku nne ya kutembelea miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya ya Ngorongoro.