MABARAZA YA HAKI YAGAWIWA KONDOO NGORONGORO
30 November 2021, 11:14 pm
Na Edward .S.Shao.
Baraza la wanawake wakifugaji Pastoral Women Council-PWC-kupitia shirika la Norway -NODAK- lagawa kondoo 168 kwa mabaraza saba ya haki na uongozi wa wanawake wilayani Ngorongoro.
Akizungumza katika hafla hiyo Novemba 29, 2021 ya ugawaji wa kondoo hao iliyofanyika katika kata ya Soit Sambu kijiji cha Mondorosi Bw.Lemweli Kileo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Ngorongoro amesema, wale wote walionufaika na kondoo katika mabaraza yao waende kuwatunza vizuri kwa faida yao na familia zao,huku akiongeza kuwa ushirikishwaji baina ya mama na baba wakati wakuuza mifugo hiyo ni jambo lakuzingatiwa ili kuepuka migongano ndani ya familia.
Naye Bw.Timothy Ole Yaile mratibu wa mradi huo wa usawa-ERISIO- kutoka shirika la PWC amesema wamefanikiwa kununua kondoo 528 kwa wilaya ya Longido na Ngorongoro iliyogharimu Milioni Sitina na tatu-63-, aidha ameongeza kuwa lengo la ugawaji huo ni kuwapa motisha mabaraza ya haki na uongozi wa wanawake ili waweze kupata nguvu na ari yakufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi.
Bi.Nairoshi Ngoitiko mkazi wa kijiji cha Kirtalo amesema mabaraza hayo yamewasaidia katika kuwaelimisha wanawake namna yakuweza kuzitetea haki zao, namna yakumiliki mifugo pamoja na kuwatetea watoto wanaolazimishwa kuolewa wakiwa wadogo.
Jumla ya vijiji saba kutoka katika kata tano wamenufaika na mradi huo,ambavyo ni kijiji cha Njoroi kata ya Ololosokwan,Mondorosi na Kirtalo kata ya Soit Sambu,cha Sukenya na Oloipiri kata ya Oloipiri, cha Sakala kata ya Orgosorok na cha Olosoito kata ya Maaloni na ni katika kila baraza lenye watu 24 wamepata kondoo mmoja mmoja kila mjumbe.