Baraza la madiwani lapendekeza chuo kuitwa jina la OLenasha .
8 November 2021, 1:02 pm
Na Edward Shao.
Baraza la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro lapendekeza chuo cha ualimu kinachojengwa katika kata ya oloipiri Kijiji Cha Orkuyaine tarafa ya loliondo wilayani Ngorongoro kiitwe jina la aliyekuwa naibu waziri uwekezaji ofisini ya waziri mkuu WILLIAM TATE OLE NASHA aliyefariki dunia September 27,2021.
Akisoma taarifa ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa wakati wa utawala wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ngorongoro na naibu waziri wa uwekezaji katika ofisi ya waziri mkuu William Ole nasha katika Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021-2022 uliofanyika hii leo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya, mwenyekiti wa Baraza ilo MH Emmanuel Shangai ameomba Baraza liazimie chuo cha ualimu kinachojengwa eneo la Orkuyaine na baadhi ya Barabara viitwe jina la Ole Nasha Kama kuenzi juhudi zake kipindi akiwa hai.
Ameongeza kuwa Katika kipindi Cha utawala wa Ole nasha utekelezaji wa miradi ya maendeleo umeongezeka kutoka kiasi cha shilingi 546,078,000 kilichotolewa mwaka 2015/2016 Hadi kufikia kiasi cha shilingi 91,301,581,587 kwa mwaka 2020/2021,aidha kwa miezi miwili pekee ya mwaka wa fedha 2021/2022 tayari halmashauri imepokea kiasi cha shilingi 481,130,182.01 na Awana budi kuenzi juhudi za Ole nasha.
Ameitaja miongoni mwa miradi mikubwa ya kihistoria aliyoitekeleza marehemu William Ole nasha tangu kuanzishwa kwa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ni pamoja na mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya,ujenzi wa Barabara ya lami km 49 kutoka wasso Hadi Sale,na ujenzi wa vituo vya afya Sakala,Osinoni,Samunge,Arashi pamoja na Sale.
Hayati William Ole Nasha Alizaliwa Mei 27,1972 na alifariki dunia September 27.2021 nyumbani kwake jijini Dodoma kwa shinikizo la damu alipokuwa ametoka mkoni Arusha kwa ziara ya kikazi na alizikwa kijijini kwake kata ya Kakesio Kijiji Cha Osinoni wilayani Ngorongoro October 02,2021