Dc Ileje awapongeza wananchi wa Itale kulinda Misitu
October 7, 2023, 7:37 am
Na Denis Sinkonde, Ileje
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe Farida Mgomi amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Itale Kata ya Itale wilayani humo Kwa kufuata sheria na kanuni za kulinda utunzaji wa mazingira hususani Msitu wa Itale na Iyevya Balendo.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kijijini hapo kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 6,2023 ulioandaliwa na ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shamba la Miti Iyondo Mswima Kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji mazingira na kujiepusha na uchomaji moto kwenye misitu.
Mgomi amesema utunzaji wa mazingira uwe endelevu kwa kutumia kamati iliyoundwa kupitia wakala wa Uhifadhi wa Misitu kwa kufuata sheria mama ambayo ni katiba kwa kuyalinda ili kulinda uoto wa asili.
sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi