Ileje FM
Ileje FM
June 18, 2025, 1:17 pm

Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa ya asilimia ya mikopo inayotolewa na hamashauri mji Tunduma kwa lengo la kuinua uchumi wao.
Na:Denis Sinkonde
Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilaya ya Momba Mkoani Songwe kwa kipindi cha uongozi wa serikali ya Awamu ya sita imetoa kiasi cha zaidi ya Bilioni 1.9 kwa vijana ikiwa ni mikopo ya asilimia 10% kutoka mapato ya ndani.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Momba Elias Mwandombo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Tunduma mbele ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed kawaida amesema kuwa wananchi wa mkoa wa Songwe wanampongeza na kumshukuru Rais Samia kwa fedha nyingi alizozitoa kwaajili ya maendeleo ya mkoa huo zikiwemo fedha kwaajili ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalumu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe Ladiwil Mwampashi amemuomba Kawaida kufikisha kilio cha Barabara ya njia nne katika mji wa Tunduma ili kuweza kurahisisha shughuli za usafishaji na biashara.
Akiongea na wananchi wa Tunduma Mkoani Songwe kwenye mkutano wa huo Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Mohamed Kawaida amesema uchaguzi hapa nchini ni kama kifo hauepukiki na kuongeza kuwa chama chake tayari kimejiandaa kunadi ilani yake ili kupata ridhaa ya Watanzania.
Kawaida ameongeza kuwa chama cha Mapinduzi kinajiamini kuelekea kwenye uchaguzi kwasababu kinayo mambo mengi ya kuwaeleza wananchi huku mengine wakiwa wanayaona wenyewe.
