Ileje FM
Ileje FM
May 26, 2025, 1:13 pm

Na Denis Sinkonde
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Songwe kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Augustino Senga amesema kufuatia zoezi la kitaifa la uchaguzi mkuu linalotalajiwa kufanyika October mwaka huu ana imani Songwe itavuka salama ambapo amewataka askari kujikita kutoa elimu kwa wananchi na wanasiasa.
Kamanda Senga ametoa kauli hiyo ameitoa wakati wa kuwavisha vyeo askari 62 wa vyeo mbalimbali kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Camilius Wambura amesema miongoni mwa mambo waliofundishwa ni wajibu wa polisi katika kipindi hiki huku akiwataka kwenda kutenda haki.
Kamanda Senga amewataka maaskari hao kwenda kwa wananchi kuwapatia elimu ili khakikisha wanapewa elimu hususani ya uchaguzi kulekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kwa upande wao askari waliovishwa vyeo vipya wameahidi kutumia nafasi zao ikiwepo vyeo vipya sambamba na kuwafikia wananchi kuwapa elimu.
Sauti askari waliovishwa vyeo vipya
