Ileje FM

Wananchi 4700 Iseche kunufaika na mradi wa maji safi

May 30, 2024, 11:46 am

Kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Iseche wilayani Songwe Mkoani Songwe{picha na Denis Sinkonde}

Na Denis Sinkonde,Songwe

Wananchi wa kijiji cha Iseche kilichopo Wilayani Songwe Mkoani Songwe wameondokana na adha ya kutumia maji yasiyo safi na salama ambayo awali walikuwa wanayapata kutoka mto songwe na kusababisha kupata magonjwa ya tumbo kutokana na matumizi ya maji yasiyo salama.

Mradi wa maji wa iseche umetekelezwa kwa gharama ya Shillingi Millioni 310 huku wananchi zaidi ya 4700 wakinufaika na mradi huo ambao tayari umeanza kutoa huduma ya maji safi na salama.

Kufuatia upatikanaji wa mradi huo wawakilishi wa wananchi pamoja na wananchi wamesema ukamilishaji wa mradi huo wa maji utakuwa na manufaa kwa wananchi kutokana na adha ambayo ilikiwa ikiwakabili wananchi hao kwa kipindi kirefu.

Sauti ya wananchi wa Iseche…………………

Mbunge wa jimbo la Songwe Philipo Mlugo amesema baada ya wananchi kufikiwa na  mradi huo ametoa msaada wa kuongeza vituo vya kuchotea maji.

Sauti ya mbunge wa Songwe Philipo Mlugo………………………

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Solomoni Itunda amesema

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Songwe Solomoni Itunda………………………….

Mkuu wa Mkoa Songwe Daniel Chongolo amesema serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha wananchi wake wanapata maji yaliyo safi na salama ambapo amewajengea mradi wa iseche ikiwa ni adhma ya kumtua ndoo mama kichwani.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe Danieli Chongolo…………………

Mkuu wa Mkoa Daniel Chongolo ameendelea na ziara katika Wilaya hiyo kwa siku tatu ambapo tayari ameshafanya ziara katika Wilaya ya Ileje na Halmashauri ya Wilaya ya Momba tayari.

katika habari picha mkuu wa mkoa wa Songwe Danieli Chongolo akiangalia kituo cha maji ambacho amefungua mradi wa maji katika kijiji cha Iseche{Picha na Denis Sinkonde}