Wananchi wachimba mashimo na kujisaidia kwa kukosa vyoo
May 10, 2024, 2:49 pm
Na Denis Sinkonde, Songwe
Jumla ya kaya 128 kati ya 320 katka Kijiji cha Mkutano Wilaya ya Momba mkoani Songwe hazina vyoo, huku kaya 34 pekee ndizo zenye vyoo bora sawa na asilimia 17.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu mara baada ya kufanya zoezi la ukaguzi wa vyoo bora kwa kupita nyumba kwa nyumba kijijini hapo.
Dkt Kasululu amewapongeza wenyeviti wa vitongoji kwa kuzitambua kaya ambazo hazina vyoo ambapo wamezibaini kaya ambazo hazina vyoo.
Aidha Dkt Kasululu amesema wananchi hawa wanachimba mashimo vichakani kwa ajili ya kujisaidia na kufukia kila siku kwa kukosa vyoo.
“Katika ukaguzi huu hatujabahatika kukuta vinyesi vichakani bali tumekuta wananchi wanajisaidia vichakani kwa kuchima mashimo,”amesema Dkt. Kasululu
Sauti ya mganga mkuu mkoa wa Songwe Dkt. Boniface Ksululu
Julias Sanane mwenyekiti wa kijiji hicho amekiri kijiji kaya nyingi kukosa vyoo hali ambayo inaweza sababisha mlipuko wa magonjwa kutokana na ukosefu wa vyoo bora.
Sauti ya mwenyekiti wa kijiji Julias Sanane
Nao baadhi ya viongozi wa dini ambao walihudhuria ukaguzi wa vyoo kwenyekijiji hicho wamesema.
Sauti za viongozi wa dini………………….