Rc Songwe akemea wananchi kuuziwa vitambulisho vyua Nida
May 1, 2024, 8:00 am
Na Denis Sinkonde,Songwe
Viongozi wa serikali za vijiji na mitaa mkoani Songwe wametahadhirishwa kutowauzia wananchi vitambulisho vya Uraia(NIDA) watakaobainika kuchukuliwa hatua kali.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itale kata ya Itale Mkuu wa Mkoa huo Daniel Chongolo leo Aprili 30,2024 amesema kutokana na mkoa huo kupakana na nchi mbili Zambia na Malawi viongozi hao wanatakiwa kujiepusha na tamaa ya kuwauzia wananchi vitambulisho vilivyotolewa bure kwa wananchi.
Chongolo amesema mkoa huo umepokea vitambilisho 365,000 ambavyo vitagawiwa bure kwa wananchi waliojiandikisha hivyo kiongozi atakayebainika kuwatoza wananchi kwa gharama yoyote atashughulikiwa.
Amewaonya viongozi hao kuacha tabia ya kuwapa vibali wananchi kutoka nchi jirani kwa lengo la kupata vitambulisho vya uraia kwani inahatarisha usalama wa nchi pamoja na kupunja keki ya watanzania ikiwepo upatikanaji wa mbolea ya ruzuku.
“Acheni kuwaruhusu wananchi wasio raia wa Tanzania kuwapa vibali vya uraia sambamba na kuwapa upenyo wahamiaji haramu kupata utambulisho hivyo tukikukamata utawajibika kwa mujibu wa sheria,” amesema Chongolo.