Viongozi wa dini hamasisheni waumini wajenge mwabweni ya shule
March 18, 2024, 4:33 pm
Denis Sinkonde, Songwe
Ili kukabiliana na mimba kwa wanafunzi wilayani Ileje mkoani Songwe viongozi wa dini wametakiwa kuwahamasisha waumini wao kujitolea kujenga mabweni kwenye shule za sekondari ili kuwaondolea adha wanafunzi wa kike kufuata masomo umbali mrefu.
Hayo yamesemwa jana Machi 15, 2024 na mbunge wa jimbo la Ileje na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya Msongwe wakati akizungumza na viongozi wa dini zote wilayani humo kwa lengo la kuweka mikakati ya kuijenga wilaya hiyo.
Mhandisi Msongwe amesema wanafunzi wengi wa shule za sekondari walayani humo wanaishi kwenye mabweni ya nje “geto” na kutemebea umbali mrefu kufuata masomo hali ambayo huwapelekea kuingia kwenye vishawishi ambavyo huwasababishia kupata mimba.
sauti ya mbunge wa Ileje Mhandisi Godfrey Msongwe
kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Ileje Abdala Mayomba amempongeza mbunge huyo kuwakumbuka viongozi wa dini ambayo ni muhimu kwa taifa.
sauti ya katibu tawala Ileje Abdalla Mayomba