Wananchi Ileje waiangukia serikali ukamilishaji wa zahanati
November 9, 2023, 6:33 am
Na Denis Sinkonde, Ileje
Wananchi wa kijiji cha Mbembati kata ya Lubanda wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamejenga zahanati ya Kijijini hapo kwa nguvu zao Ili kupunguza adha ya kusafiri umbali wa km 8 kufuata huduma katika kituo cha afya Lubanda.
Wananchi hao walianza ujenzi wa zahanati hiyo mwaka 2014 kwa lengo la kuwapunguzia akina mama wajawazito ambao walikuwa wakijifungulia njiani na majumbani wakati wakifuata huduma ya uzazi kituo cha afya Lubanda ambapo awali ilikuwa zahanati.
Akisoma taarifa ya kijiji Odeni Kandonga amesema kati ya fedha hizo wananchi wamechangia milioni 15 laki sita na elfu sitini na nane, fedha ya mfuko wa jimbo ni milioni nne, na michango ya wahisani ni shilingi laki nane.
Sauti ya Odeni Kandoga
Mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi amewapongeza wananchi kwa ushiriki wao kwenye miradi ya maendeleo ikiwepo ujenzi wa zahanati na nyumba ya mwalimu kwa nguvu zao.
sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi
katika hatua nyingine wananchi wa Kijiji hicho wamewasilisha kero zao kwa mkuu wa wilaya.
sauti za wananchi wa Mbembati