DC Ileje aagiza wananchi waelimishwe matumizi sahihi ya vyandarua
November 3, 2023, 9:19 am
Na Denis Sinkonde, Ileje
Wataalam wa afya na viongozi wa serikali wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe wameagizwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya vyandarua vyenye dawa ili wajiepushe kutumia kutengenezea bustani za mbogamboga na kuvulia samaki.
Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi ametoa agizo hilo Novemba 2, 2023 wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule za msingi 87 wilayani hapa ambapo zaidi ya vyandarua elfu 19,000 vitagawiwa.
Mhe. Mgomi amesema vyandarua hivyo vimetolewa na wizara ya afya kupitia bohari ya dawa (MSD) hivyo vitumike Kwa lengo la kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Maralia kufikia mwaka 2030.
Sauti ya mkuu wa wilaya Farida Mgomi
“Wataalam wa afya hakikisheni mnatoa elimu Kwa wananchi ya matumizi sahihi ya vyandarua kwani lengo la serikali imetoa vyandarua hivyo kwa ajili ya kutokomeza malaria lakini wananchi wanatumia tofauti na maelekezo,” amesema Mhe. Mgomi.
Aidha Mhe. Mgomi amewatahadharisha wananchi kuacha kutumia vyandarua kutengenezea bustani za mbongamboga tukikunaini hatua kali zitachukuliwa kwani utakuwa unaenda tofauti na matakwa ya serikali ya kutokomeza Maralia kufikia mwaka 2030.
Akizungumza wakati wa zoezi la uzinduzi ugawaji wa vyandarua hivyo kwa wanafunzi memeja bohari wa dawa Kanda ya Mbeya Marco Masala kwaniaba ya wizara ya afya amewasihi wananchi kulala kwenye vyandarua ili kukomesha maambukizi ya Maralia.
sauti ya meneja wa MSD kanda ya Mbeya Marco Masala
Mratibu wa Maralia wilayani hapa Mkaaya Said amesema zoezi hilo litaenda kama ilivyopangwa Kwa Kila mwalimu mkuu wa shule kugawiwa vyandarua Kwa ajili ya kugawa Kwa Kila mwanafunzi na kumtaka Kila mzazi kuhakikisha mtoto wake analala ndani ya chandarua.
Mratbu wa Maralia Ileje Mkaaya Saidi