Wananchi Ileje wajitolea kujenga nyumba ya mtoa huduma wa afya
October 22, 2023, 7:40 am
Na Denis Sinkonde, Ileje
Wananchi wa kijiji cha Izuba kata ya Isongole wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe wanatarajia kumaliza ujenzi wa vyumba ya wahudumu wa zahanati ya Izuba ili kuwaondolea adha wahudumu wa zahanati hiyo kuishi mbali.
Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya Isongole Gwalusako Kapesa katika mkutano wa hadhara ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi katika kijiji cha Izuba.
Kapesa amesema baada ya serikali kulidhia zahanati hiyo kutoa huduma bila kuwepo kwa nyumba ya kuishi wananchi wakaanza kutoa michango
Akisoma taarifa ya kijiji mbele ya mkuu wa wilaya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Izuba Severina Kayange amebainisha changamoto za kijiji icho.
Kwa upande wake kaimu wa zahanati hiyo Petro Matwinga amesema wataweka bajeti ijayo ili kusaidia nguvu kazi ya wananchi.
Katika kufanikisha umaliziaji wa jengo hilo Zaidi ya shilingi million tatu zinaitajika ambapo kila mwananchi anatakiwa kuchanga elfu sita.
Sauti ya mwanahabari wetu Ester Simbeye Inafafanua zaidi.