Viongozi wasiotatua changamoto za wananchi wajitathimini-DC Ileje
October 11, 2023, 4:55 pm
Na Denis Sinkonde, Songwe
Viongozi wa kata na vijiji wilayani Ileje mkoa wa Songwe wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea pasipo kuwashirikisha wananchi kupanga vipaumbele vya miradi ya maendeleo kwenye vijiji.
Hayo yamebainishwa Oktoba 10, mwaka huu na mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mapogoro kata ya Mbebe wilayani hapa kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza wananchi baada ya kupokea kero ya viongozi kutoitisha mikutano na kutosoma mapato na matumizi.
Mgomi amesema viongozi hao lazima wasikilize kero za wananchi na kuweka ratiba za vikao kila baada ya robo mwaka.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wamewatupia lawama viongozi wa kijiji kutowashirikisha kwenye maamuzi ya kupanga shughuli za maendeleo.
sauti ya wananchi mapogoro
Akijibu shutuma za wananchi mtendaji wa kijiji hicho amesema