Mliovamia hifadhi hekta 600 za hifadhi ondokeni haraka Dc Ileje
October 4, 2023, 7:15 am
Na, Denis Sinkonde, Ileje
Wananchi vijiji vya Ndapwa kata Ngulilo wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe na Kijiji Cha Kiobo wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya wametakiwa kuondoka na kuacha na uvamizi kwenye hifadhi ya msitu Kihosa uliopo Kijiji Cha Ndapwa wilayani Ileje Kwa kufuata kanuni na Sheria za misitu.
Agizo hilo limetolewa Oktoba 3,2023 na mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Ndapwa kwenye mkutano wa hadhara kwenye kampeni ya oparesheni ya uhifadhi wa misitu uliondaliwa na ofisi ya wakala wa huduma za misitu Tanzania shamba la miti Iyondo Mswima wilayani humo (TFS).
sauti ya mkuu wa wilaya Ileje Farida Mgomi
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Iyondo Mswima lililopo Wilaya ya Ileje Jovan M Emanuel amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Ndapwa kuwa TFS itaanza zoezi la kugawa miche ya miti kwa wakazi wa eneo hilo mapema mwezi wa 12 ikiwa ni adhima ya kutekeleza dira ya uhifadhi wa mazingira lakini pia kuongeza kipato kwa wananchi.
sauti ya mhifadhi mkuu shamba la miti Iyondo Mswima Jovin Emanuel
Mwenyekiti wa kamati iliyochaguliwa Elius Cheyo amesema
sauti ya mwenyekiti kamati ya utunzaji uhifadhi wa mazingira Ndapwa Elius Cheyo