Barabara km 52.414 kulimwa kwa kiwango cha lami Ileje Samia apongezwa
September 21, 2023, 7:02 am
Na Denis Sinkonde
Askofu wa kanisa la Moraviani jimbo la Kusini Kenani Panja kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Ibungu Kata ya Bupigu ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia_Suluhu Hassan pamoja na Viongozi wengine wa Kiserikali kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Isongole- Isoko yenye urefu wa Kilomita 52.414.
Askofu ameyasema hayo wakati akikamilisha taratibu za malipo ya fidia katika Kijiji cha Ibungu ambapo amebainisha kuwa ndiyo chimbuko lake.
Pamoja na shukrani hizo Askofu Panja amemuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan afya njema na maisha marefu ili aendelee kuwatumikia wananchi wake.
Sautiya Askofu Kenani Panja
Kwa upande wake Abisai Peter Lukali ambaye ni Chief wa Ibungu amesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa maendeleo na kipato cha mtu mmoja mmoja na hivyo kuwafanya waishi kama wapo mjini.
Suti ya Chifu Abishai Lukali
Zoezi la malipo ya fidia linaratibiwa na Tanroad kwa kushirikiana na Wajumbe wa Kamati ya Usalama (W) huku jumla ya watu 312 watanufaika na malipo hayo yenye zaidi ya Shilingi Milioni 850.