Waandishi wa habari Ileje Fm wanolewa umuhimu matumizi ya kidigitali
September 16, 2023, 10:00 am
Na Denis Sinkonde
Waandishi wa habari kutoka kituo Cha Ileje FM wamenolewa namna bora ya uandishi wa habari za mitandao kwa kuzingatia miiko ya kihabari ili kuchochea mabadiliko kwenye jamii.
Wito huo umetolewa Septemba 16 ,2023 na mkufunzi kutoka mtandao wa redio za jamii Tanzania TADIO Amua Rushita wakati anatoa mafunzo ambayo yamefanyika Leo katika ofisi za redio zilizopo mji wa itumba wilaya ya ileje .
Rushita amesema kuwa utawandazi una kua kwa Kasi duniani hivyo redio za jamii hazina budi kuendana na Kasi hivyo katika kutumia mfumo wa kidigitali ambao unasaidia kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi.
Sauti ya mkufunzi Amua Rushita.
Amua ameongeza kuwa jamii inapenda vitu vizuriĀ na vitu vizuri vinavutia watu wengi ambapo amedai kuwa tunu ya waandishi wa habari ni ubunifu katika kutumia mitandao kwa ajili ya kurusha habari mbalimbali.