DC Ileje awakabidhi baiskeli wanufaika 25 mradi wa IRDO
September 15, 2023, 10:36 am
Na Sikudhani Minga
Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi amekabidhi zaidi ya baiskeli 25 kwa wananchi wa wilaya ya Ileje ambao ni wanufaika kutoka shirika lisilo la Kiserikali la Integrated Rural Development Organization (IRDO) ambalo limejikita katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwemo ukosefu wa elimu juu ya kilimo na uhifadhi wa chakula lakini pia lishe bora pamoja na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Akiongea wakati wa kukabidhi baiskeli Mgomi amewasisitiza wanufaika kuzitumia baiskeli hizo kwenye malengo tarajiwa ili kuongeza tija katika uzalishaji.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi
Andaghisye Masebo mkazi wa kijiji cha Mapogoro kata ya Mbebe wIlayani hapa ambaye ni mnufaika wa miradi mbalimbali inayoendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la IRDO ametoa shukrani za pekee na kutambua mchango wa Shirika hilo katika kuwasaidia wananchi kwenye suala zima la Lishe basa kwa watoto wadogo.
Sauti ya mwananchi Andaghisye Masebo
Shirika hilo limefanikiwa kutoa mafunzo kwa Wakulima katika lengo la kuboresha mbinu za kilimo, kuongeza upatikanaji wa chakula katika ngazi ya kaya lakini pia kuongeza uwezo wa vikundi vya wakulima katika uzalishaji wenye tija.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la IRDO Dkt. Simon Chiwanga ni kwamba tayari shirika limefanikiwa kugusa zaidi ya kaya 50 kila kijiji katika zaidi ya vijiji 11 kwenye tarafa mbalimbali za Wilaya ya ileje.