RUWASA Ileje walia na uharibifu wa mazingira
September 12, 2023, 7:51 am
Na Denis Sinkonde, Songwe
Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA wilayani Ileje mkoani Songwe walia na changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji hali inayopelekea baadhi ya miradi kutotoa maji kama ilivyokusudiwa.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa vyombo vya watumia maji wilayani hapa David Gunza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kamati ya ulinzi ya usalama wilaya juu ya usimamizi wa utoaji huduma ya maji vijijini huku akitolea mfano chanzo cha maji Malangali , Shinji na Itale.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii wa mamlaka hiyo wilayani hapa Sifa Edom ameelezea changamoto ya ulipaji Ankara kwenye vituo vya maji.
Kutokana na changamoto hiyo mkuu wa wilaya ya Ileje ameuagiza uongozi wa RUWASA wilayani hapa kuorodhesha miradi iliyokamilika na isiyokamilika lengo ni kusaidiana kwa pamoja kubaini kutatua changamoto zinazopelekea miradi hiyo kutowanufaisha wanainchi.
uongozi wa RUWASA wilayani hapa orodhesheni miradi iliyokamilika na isiyokamilika lengo ni kusaidiana kwa pamoja kubaini kutatua changamoto zinazopelekea miradi hiyo kutowanufaisha wanainchi.