watoto 20 kati ya 85 wakutwa na udumavu Ileje
October 21, 2021, 9:11 am
Watoto 20 kati ya 85 wamekutwa na udumavu katika kiijiji cha Igumila wilayani Ileje mkoani Songwe baada ya kupimwa na wataalamu wa afya wakati wa kutoa elimu juu ya umuhimu wa lishe ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa oktoba 23 mwaka huu mkoani Tabora.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho afisa lishe wilayani hapa Mary Aloisi amesema wazazi na walezi wilayani hapa hawana elimu juu ya umuhimu wa lishe hivyo kuwasihi kuwa ajenda ya familia kuwapatia watoto vyakula vinavyotakiwa na si kuwanywesha pombe za kienyeji.
Afisa huyo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanzazingatia suala la lishe kama ajenda ya familia ili kuepusha udumavu unaowakabili watoto wengi mkoani hapa licha ya kuwa na unazalisha vyakula vingi.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika vijiji vya Ibeta,Kikota na Mlale na kuendelea katika vijiji
vingine likilenga kutoa elimu kujua ukuaji wa watoto na kutoa ushauri kwa watoto.
Magreth Simbeye na Juma Msyaliha wamesema elimu waliyoipata juu ya lishe itawasaidia kuondoa udumavu kwa watoto wao na kuwasihi wanaume kushirikiana wake zao kuandaa lishe kwa ajili ya matumizi ya watoto wao.