Songwe kutimiza ndoto ya Mh. Samia Januari 2022
October 15, 2021, 12:07 pm
Mkoa wa Songwe umetangaza mkakati mahususi wa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya msingi itakayowezesha kufunguliwa na kupokea wanafunzi kwa shule ya wasichana ya Mkoa inayojengwa katika eneo la Myunga,Wilayani Momba mkoani Songwe.
Azimio hilo lilifikiwa hivi karibuni kwenye kikao cha maendeleo ya Elimu Mkoa kilichoketi chini ya Katibu Tawala (RAS) Misaile Mussa na kufanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkoa.
Misaile amwesema miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kila Halmashauri ya Mkoa huo kuchangia kiasi cha shilingi milioni 30.
Afisa Elimu Mkoa wa Songwe, Mwl. Juma Kaponda amesema kwa jinsi Rais Samia alivyoleta fedha za ujenzi wa madarasa 291 kwa Mkoa wa Songwe, Halmashauri haziwezi kushindwa kutoa fedha Milioni 30 ambazo ni sawa na chumba kimoja cha darasa na ofisi tu.
Kuanza kwa Shule hii ni kukamilisha ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka wanafunzi wa kike wa Songwe wasome bila bukuza.