Adhana FM

Walimu wa Takwimu wahimizwa matumizi ya mfumo wa kuweka taarifa za shkuli wa SIS Kasazini Unguja

20 August 2026, 1:07 pm

Na Mwandishi Wetu,

Mkokotoni Asifa elimu mkoa kaskazini Unguja, Subira Vuai Abdallah amekutana walimu wa takwimu kutoka skuli za mkoa huo ili kutatua changamoto za matumizi ya mfumo wa kuweka taarifa wa SIS.

Akizungumza na walimu, Afisa elimu amewataka walimu kubadilika na kwenda sambamba na amtumizi ya teknolojia kulingana na wakati uliopo ili kuisaidia wizara ya elimu kuwa na taarifa sahihi za mahudhurio ya kila siku ya walimu na wanafunzi.

Amesema bado kuna changamoto kubwa kwa walimu wa takwimu kutokuweka mahudhurio kwenye mfumo wa SIS ambao wilaya za mkoa wa kaskazini ni za mwisho katika suala la taarifa za mahudhurio.

Akiwakumbusha walimu matumizi ya mfumo wa SIS, Afisa takwimu wa Wilaya Kaskazini A, Mwalimu Ramadhan Kombo Farhan amewapitisha walimu kwenye vipengele vya mahudhurio ili kuondoa tatizo la kutokuweka mahudhurio kwenye mfumo.

Kwa upande wake Afisa takwimu wilaya Kaskazini B Mwalimu Shaib Abdallah Hmbali amewahimiza walimu wakuu kutenga fungu maalumu la matumizi ya vifurushi vya mtandao ili watakwimu waweke taarifa za kila siku kwenye mfumo wa SIS.