Adhana FM

Wenyeji 960 wapewa ajira kwenye mradi wa ujenzi wa barabara Zanzibar.

9 January 2024, 6:54 pm

Na Najat Omar

Kampuni ya CCECC inayojenga barabara za mjini na vijijini visiwani Zanzibar, imewapatia ajira wazanzibar wapatao 960 kwenye mradi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Serena Zanzibar, Mkurugenzi wa CCECC Afrika Mashariki Zhang Junle amesema mradi huo wa miaka mitatu umetoa fursa za ajira na ujuzi kwa wakandarasi wazawa na wataalam kutoka kanda nyengine.

“Sio tu ajira bali pia suala la kuwaongezea maarifa na utaalamu kwa wazawa limezingatiwa kwenye mkataba wa ujenzi wa barabara hizo “ amefafanua Junle.

Kuhusu wananchi waliopitiwa na mradi huo kwenye makazi na mashamba yao, suala la fidia linalozingatiwa kwani ni miongoni mwa masharti ya mradi.

“Tunapokea tathmini kutoka Serikalini nasi tunalipa kwa mujibu wa orodha na malipo yalivyopanga ila kama kuna malalamiko ya kutokulipwa basi tutashungulikia na kuwapa watu haki zao” Ameongeza Meneja Mradi wa Kampuni ya CCECC – Zanzibar Xiong Yun Xu.

Mkataba wa ujenzi wa barabara za mijini na vijini pamoja na madaraja mawili makubwa ulisainiwa mwaka 2022 na kutarajiwa kumalizika 2025 huku barabara 45 zikitarajiwa kujenga ambazo kwa ujumla wa barabara hizo zinao urefu wa kilomita 100.9 huku mradio huo ukigharimu shilingi bilioni 275.