Adhana FM

Makamu wa Kwanza Rais Zanzibar akutana na balozi mdogo wa Uingereza nchini

10 August 2023, 1:09 pm

Balozi Mdogo wa Uingereza akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

Viongozi hao wamekutana nakuzungumzia Maridhiano ya kisiasa Zanzibar

Na Afisi ya Makamu wa Kwanza

Makamu wa Kwanza Wa Rais Wa Zanzibar Othman Massoud Othman aesema kwamba kuanza kwa vikao vya Kamati ya Pamoja ya Maridhiano ya Kisiasa Klkati ya Chama Cha Act -Wazalendo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni hatua muhimu ya kutia moyo na ya kuleta matumaini ya kuwepo na kuendelea  mjadala  wa masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali mwema wa Zanzibar.

Othman ameyasema hayo nyumbani kwake Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar, alipokutana na balozi mdogo wa Uingereza nchini Tanzania Rick Shearn, aliyetaka kujua pamoja na mambo mengine maendeleo ya kamati hiyo ya pamoja iliyoundwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Amesema kwamba hivi sasa kamati hiyo imeanza vikao vyake kwa kujadili maeneo na agenda  muhimu  na makhususi  na namna  ya utaratibu bora utakaotumika katika kuyajadili masuala muhimu katika agenda hizo ili kufikia muafaka kwa malengo yaliyokusudiwa ya mustakabali wa Zanzibar na watu wake.

Sauti ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

Aidha Othman amesema anaamini kwamba katika vikao hivyo vya awali maeneo yote muhimu yanayohitaji kufanyiwa mabadiliko na mageuzi makubwa yameainishwa kwa kuwasilishwa na kujadiliwa  kwa pamoja katika kutafuta maslahi bora ya Zanzibar na  watu wake.

Makamu amefahamisha kwamba kuwepo kwa hatua hiyo ni fursa muhimu kwa Zanzibar katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025 katika kufanya mabadiliko na mageuzi yanayotarajiwa na wananchi wa Zanzibar katika kuweka matumani ya mustakabali wa nchi yao.

Amesema majadiliano hayo ya awali yamegusa katika maeneo muhimu yote likiwemo suala la mageuzi na mabadiliko  katika masuala ya uchaguzi ikiwemo tume inayosimamia uchaguzi ili kuifanya kuwa taasisi imara kwa maendeleo na mustakabali mwema wa Zanzibar.

Amefahamisha kwamba agenda ya mausuala ya uchaguzi inaendelea kama jambo muhimu katika misingi ya mjadala huo kwa kuwa unalenga maisha ya Wazanzibar, biashara kwa Zanzibar, na uwekezaji kwa maendeleo ya nchi.

Akizungunzia suala la katiba, Othman amesema kwamba hilo ni suala la muungano, lakini linagusa maendeleo ya masuala kadhaa ya Zanzibar moja kwa moja ambapo yapo masuala mengi yanayohitaji kufanyiwa mageuzi katika usimamizi na uendeshaji wake ikiwemo suala la haki, jinai na uchaguzi wa wabunge nw Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naye Balozi Mdogo wa  Uingereza nchini Tanzania  Rick Shearn alitaka kufahamu iwapo suala la Katiba Mpya ya Jamhuri ys Muungano wa Tanzania pia linaweza kuathiri mustakabali wa Zanzibar  katika uchaguzi ujao wa nwaka 2025 na utekelezaji wa masuala mbalimbali ikiwemo  uchaguzi wa Zanzibar.

Sauti ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar